Zahera ahofia kucheza mechi ya kirafiki katikati ya ligi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Sep 2018
Zahera ahofia kucheza mechi ya kirafiki katikati ya ligi
Huenda ule mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Singida United uliokuwa umepangwa kupigwa mkoani Kigoma keshokutwa umefutwa.

Awali Yanga ilitarajiwa kusafiri kwenda mkoani humo lakini kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Tanzania, Mwinyi Zahera amegoma timu yake kucheza mchezo wa kirafiki katikati ya ligi.

Zahera ambaye amerejea kwao DR Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa, ameagiza kikosi chake kiendelee na mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Stand United utakaopigwa uwanja wa Taifa Septemba 16.

Yanga iliyokuwa mwenyeji wa mchezo huo, ilipanga kuutumia kujiongezea mapato kwa kuupeleka mkoani Kigoma ambako ni muda mrefu mashabiki wake wamekosa kuzishuhudia timu za ligi kuu.

Lakini hofu ya kuongeza majeruhi kikosini imemfanya bosi huyo wa benchi la Ufundi kuugomea mchezo huo.

Yanga tayari inakabiliwa na wachezaji majeruhi kama Juma Abdul, Heritier Makambo, Mohammed Banka na Juma Mahadhi.

Baadhi ya wachezaji tayari wameanza mazoezi mepesi huku wakiendelea na matibabu kuhakikisha wanakuwa tayari kuitumikia Yanga kwenye michezo ijayo ya ligi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’