Zahera kuamua hatma ya Chirwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2018
Zahera kuamua hatma ya Chirwa
Uongozi wa Yanga hauna kinyongo na aliyekuwa mshambuliaji wake Obrey Chirwa ambaye ameonyesha nia ya kutaka kurejea Jangwani baada ya kuamua kuvunja mkataba wake na klabu ya Nogoom El Mostakbal inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri.

Chirwa anataka kuachana na Nogoom El Mostakbal baada ya klabu hiyo kushindwa kumlipa fedha za usajili kwa mujibu wa makubaliano yao.

Taarifa ya Chirwa kutaka kurejea Yanga iliibuka mapema wiki hii baada ya mshambuliaji huyo kuwatumia viongozi wa Yanga ujumbe wa sauti akiomba kurejea hata kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Habari za Uhakika ni kwamba Kamati ya Usajili ya Yanga iko tayari kumpokea mshambuliaji huyo msumbufu kama Kocha Mwinyi Zahera ataridhia asajiliwe.

Wengi wanaamini safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo sasa inamtegemea Heritier Makambo itakuwa hatari zaidi kama Chirwa ataongezwa.

"Makocha wamesema ukiacha tabia yake, lakini kama dili hilo litafanikiwa Chirwa anaweza kuongeza uhai kwa Makambo kwa kumwongezea makali zaidi ya kufunga," amenukuliwa mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Usajili

β€œKazi ya kuifanyia tathimini pacha hiyo imeanza, unajua Chirwa ni mbishi kwa mabeki na anajua kupambana hivyo, wakati akiwania mipira kazi ya Makambo itakuwa ni kufunga tu. Ngoja tutaona hatima yake kwa Zahera,” alisema bosi huyo
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’