Tuiunge mkono Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2018
Tuiunge mkono Stars
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kesho Jumamosi inashuka kwenye uwanja wa Mandela jijini Kampala kuikabili Uganda Cranes katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika nchini Cameroon mapema mwakani.

Stars iko kundi L sambamba na Uganda, Lesotho na Cape Verde.

Uganda inaongoza kundi hilo kufuatia ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya Cape Verve katika mchezo wake wa kwanza wakati Stars na Lesotho zilitoka sare ya bao 1-1 hivyo kugawana alama moja moja.

Mara ya mwisho kwa Tanzania kushiriki michuano ya AFCON ilikuwa mwaka 1980 lakini inaweza kuirudia historia hiyo mwaka huu kama itazichanga vyema karata zake.

Kwa mara ya kwanza Stars imepangwa katika kundi ambalo 'halitishi' sana kwani kundi hilo linatoa nafasi karibu sawa kwa kila timu.

Mchezo wa kesho dhidi ya Uganda una umuhimu wa kipekee kwa Stars kwani utatoa mwanga juu ya hatma ya Stars kwenye michuano hiyo.

Uganda ndio inapewa nafasi kubwa ya kufuzu katika kundi hilo kwa kuwa hata katika viwango vya FIFA inashika nafasi ya juu zaidi kuliko wapinzani wake.

Lakini hilo haliitishi Stars ambayo imekuwa ikiimarika siku hadi siku kutokana na kuongezeka kwa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Kwa mara ya kwanza kikosi cha Stars kilichokwenda Uganda kina wachezaji tisa wanaosakata kabumbu nje ya Tanzania.

Matokeo ya ushindi au hata sare kwa Stars kesho yataiweka Tanzania kwenye nafasi nzuri kabla ya timu hizo kurudiana kwenye michezo ya mzunguuko wa pili ambapo mchezo dhidi ya Uganda utapigwa uwanja wa Taifa.

Jambo la msingi kwa Watanzania wote ni kuiunga mkono Stars kwani ndio timu inayotuunganisha sote.

Kwenye mitandao ya kijamii kumejitokeza baadhi ya mashabiki hasa wa Simba bila aibu kujinasibu kuwa wataiunga mkono Uganda eti kwa kuwa wachezaji wa timu yao waliondolewa kikosi cha Stars na kocha Emmanuel Amunike.

Ni muhimu uamuzi wa kocha ukaheshimiwa.

Sababu za wachezaji hao kuondolewa kikosini ziliwekwa wazi. Na si hao pekee, kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' nae aliondolewa kikosini kwa sababu hizohizo lakini mashabiki wa Yanga hawajasikika wakisema wataikacha Stars.

Moja ya changamoto zinazotufanya hatusongi mbele kimataifa ni hii tabia ya kuweka mbele vilabu vyetu hata linapokuja suala la timu ya Taifa.

Hii tabia ya kulazimisha kwamba wachezaji wa timu yetu lazima wawe kwenye timu ya Taifa au lazima wacheze bila ya kujali viwango na misimamo ya kocha imekuwa ikitugharimu sana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’