Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike amesema wamekwenda Uganda kuchukua alama zote tatu ili kujiweka katika mazingira mazuri katika kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON 2019.
Kocha huyo aliyetamba zaidi na timu ya Taifa ya Nigeria wakati akicheza mpira amesema timu yake imejipanga kikamilifu kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
"Kama unakumbuka wakati nacheza soka, nilikuwa mchezaji ambaye ukimtazama unajua anatafuta matokeo, nipo hivyo hadi sasa, nimekuja kushinda," Amunike amewaambia waandishi wa habari jijini Kampala leo.
Naye nahodha msaidizi wa Stars Himid Mao amesema wanaiheshimu Uganda na wanatambua ni timu ambayo iko kwenye kiwango bora wakati huu.
Lakini wao wamekwenda Uganda kutafuta matokeo hivyo anaamini mchezo huo utakuwa mzuri na wenye ushindani kutoka kwa kila upande.

ADVERTISE HERE