Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewataka wapenzi na wanachama wa klabu ya Yanga kudumisha umoja na ushirikiano ili kufanikisha malengo.
Akizungumza na Wanachama wa Yanga kwenye Tawi la Kariakoo visiwani Zanzibar leo, Mkwasa amewataka wanachama kulipia ada zao kwa wakati.
Amesisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kuijenga Yanga yenye nguvu na kusisitiza umuhimu wa kuichangia klabu kwa hali na mali ili kuwezesha mafanikio yanayohitajika.
"Tunahitaji kusaidia kuiendeleza Yanga. Sisi peke yetu hatuwezi," amesema Mkwasa.
"Msifikiri huku kuna hela nyingi, sisi tunajitolea tu kwani kama hatukupata hela zamani basi hatuwezi kuzipata Yanga sasa."
Naye Mwenyekiti wa Tawi la Kariakoo Sammy Masoud amesema wanachama wa Yanga Zanzibar wameridhishwa na maandalizi ya klabu kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba August 23.
Tazama sehemu ya mkutano huo kwenye ukurasa wa Videos.

ADVERTISE HERE