Mashabiki, Wanachama ndio waliipeleka Yanga Rwanda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
11 Sep 2018
Mashabiki, Wanachama ndio waliipeleka Yanga Rwanda
Zoezi la kuichangia Yanga lililoanzishwa na uongozi mwezi uliopita limekuwa na mafanikio kwani michango hiyo imewezesha kukamilisha baadhi ya mambo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omari Kaya amesema kupitia michango hiyo Yanga imeweza kusafiri kwenda nchini Rwanda kumalizia mchezo wa mwisho wa michuano ya kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports mwishoni mwa mwezi wa nane.

Lakini pia michango hiyo ilitumika kuigharamia timu ilipokuwa nchini Rwanda na kuweza kurejea salama.

Hatua hii imeleta maana halisi ya timu ya wananchi na hakika WanaYanga wanastahili kujipongeza kwa mafanikio haya na ni muhimu kuendelea kuchangia timu ili iweze kufanya vizuri kwenye ligi.

Uongozi wa Yanga umeweka bayana kuwa zoezi hili ni endelevu kwa wakati huu ambao klabu hiyo kongwe zaidi nchini iko kwenye michakato ya kuifanya iweze kujitegemea.

“Wengine wanaweza kudharau hii michango, lakini kwa wanaochangia wanatakiwa kutambua hii ni hatua nzuri kwa klabu hasa baada ya kufanikisha kugharamia safari yetu ya Rwanda,” Kaya amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

“Tulipokwenda Rwanda mimi najua ni jinsi gani hizi fedha zilitumika kuhakikisha timu inaenda na kurudi salama hapa nchini.

"Haya ni mafanikio ya nguvu ya wanaotuchangia na tunawashukuru wote waliojitoklea na tunaomba waendelee.”

“Michango hii kama itaendelea nafikiri inaweza kuisaida sana timu hata katika mechi za ligi na hili hata wachezaji wanalitambua na wameniahidi watapambana kulipa fadhila kwa wanachama na mashabiki wao.”
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →