Yanga yasaka rekodi ya kipekee Uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Sep 2018
Yanga yasaka rekodi ya kipekee Uwanja wa Taifa
Keshokutwa Jumapili kikosi cha Yanga kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Stand United huo ukiwa ni mchezo wake wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu.

Yanga ilipata ushindi kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa August 23.

Baada ya kuukosa ubingwa msimu uliopita, Yanga imedhamiria kurejesha ubingwa mahala pake kwa mara ya 28 msimu huu.

Ili kuweza kufanikisha hilo, mabingwa hao wa Kihistoria ni lazima waitumie vyema michezo itakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa kwa kuibuka na ushindi.

Mchezo dhidi ya Stand United utakuwa mmoja wa michezo 11 mfululizo ambayo Yanga itakipiga kwenye dimba la Taifa kabla ya kuanza kuzunguuka mikoani.

Ikiwa tayari imeshinda mchezo mmoja kwenye uwanja huo msimu huu, kama itafanikiwa kushinda michezo hiyo 11 itafikisha alama 36 na huo utakuwa mwanzo mzuri wa kampeni ya kuurejesha ubingwa Jangwani.

Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam tayari kuikabili Stand United.

Yanga imeimarika baada ya kurejea kikosini wachezaji waliokuwa timu ya Taifa Beno Kakolanya, Gadiel Michael na Andrew Vicent huku Kelvin Yondani, Abdallah Shaibu na Juma Abdul wao wakirejea baada ya kupona majeraha.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’