TAKUKURU yaahidi donge nono kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa Hans Poppe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Sep 2018
TAKUKURU yaahidi donge nono kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa Hans Poppe
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe ambaye pia anahusika na masuala ya usajili anatafutwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) akituhumiwa na makosa ya kutoa rushwa.

Mapema leo, TAKUKURU ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikiwataka Hans Pope na Mkurugenzi wa kampuni ya Ranky Infrastructure & Engineering, Franklin Lauwo, wajisalimishe wenyewe katika ofisi zao kutokana na tuhuma za makosa mbalimbali ya rushwa yanayowakabili.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Takukuru Brigedia Jenerali John Mbungu, amesema juhudi mbalimbali za kuwatafuta watu hao zimegonga mwamba hivyo wanatakiwa watii amri na kujisalimisha wao wenyewe.

Naibu Mkurugenzi huyo amesema Poppe anatuhumiwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuhusiana na malipo ya kodi.

Kati ya Machi 10,2016 na Septemba 30, 2016, mshitakiwa huyo akishirikana na washitakiwa wenzake, Evans Aveva na Geofrey Nyange walitoa maelezo ya uongo kwenye ofisi za TRA, kwamba klabu ya Simba imenunua nyasi bandia kutoka Ninah Guangzhou Trading Limited kwa thamani ya dola za kimarekani 40,577.

β€œUkweli ni kuwa nyasi hizo zilinunuliwa dola za kimarekani 109,499 lengo ikiwa ni kukwepa kulipa kodi ya mapato sahihi kwa TCRA,” ameeleza.

Amesema kwa upande wa Lauwo anashtakiwa kwa kosa la kufanya biashara ya ukandarasi na aliupata kwa njia ya rushwa kwa sababu hakuwa na sifa na sio mkandarasi ambae amesajiliwa na bodi ya makandarasi nchini.

β€œKati ya Machi na Septemba 2016, mshitakiwa alifanya kazi ya ukandarasi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa klabu ya Simba uliopo Bunju, Kinondoni kwa thamani ya zaidi ya bilioni mbili wakati hajasajiliwa na bodi ya makandarasi, kisheria kufanya kazi hiyo,” amefafanua.

Aidha Brigedia Mbungu ameongeza kwamba mtu yeyote atakayesaidia kutoa taarifa za ukweli zitakazosaidia kupatikana kwa washitakiwa hao atapewa zawadi nono.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’