Mkakati wa Zahera kuirejesha Yanga anga za Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Sep 2018
Mkakati wa Zahera kuirejesha Yanga anga za Kimataifa
Papi Tshishimbi, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Heritier Makambo na Klaus Kindoki ndio wachezaji wa kigeni wanaoitumikia Yanga msimu huu.

Wakati TFF ikiwa imeruhusu vilabu kusajili wachezaji wa kigeni ambao idadi yao inaweza kufika kumi, Yanga bado ina nafasi ya wachezaji watano.

Katika jitihada za kuhakikisha anaimarisha kikosi chake, Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera tayari ameweka wazi baadhi ya wachezaji ambao anataka watue Jangwani wakati wa dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa siku 60 zijazo.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanahitajika na kocha Zahera watue Yanga dirisha dogo la usajili;

Rwabutaye Abdoul

Rwabutaye Abdoul ni nahodha wa kikosi cha Rayon Sports. Beki huyo kisiki alionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo dhidi ya Yanga na kuwafanya mabosi wa usajili wakiongozwa na Hussein Nyika wamuwahi haraka kufanya nae mazungumzo ya awali.

Rwabutaye bado ana mkataba na Rayon lakini ameonyesha kuwa tayari kutua Jangwani kama makubaliano baina ya timu yatafikiwa.

Yanick Bangala Litombo

Yanick anakipiga katika klabu ya AS Vital ya huko DR Congo. Huyu angeweza kutua Jangwani wakati wa usajili wa dirisha kubwa kama mambo ya kiuchumi yangekuwa sawa.

Inaelezwa beki huyu ambaye yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo tayari alishakubali kutua Jangwani baada ya kushawishiwa na Zahera.

Fabrice Ngoma

Huyu ni kiungo ambaye anakipiga katika klabu ya AS Vital pia. Kulingana na kocha Mwinyi Zahera, Ngoma ameonyesha utayari wa kutua Jangwani hasa ikizingatiwa mkataba wake na timu yake unaelekea ukingoni.

Ben Malongo

Huyu ni mshambuliaji kutoka klabu ya TP Mazembe ambaye amependekezwa na kocha Zahera. Naye yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo.

Uwepo wa kocha Zahera kwenye kikosi cha DR Congo kunaweza kuinufaisha Yanga kwani amekuwa na nafasi adimu ya kuzungumza na wachezaji hawa moja kwa moja.

Ahmed Toure

Huyu ni Straika wa Kimataifa wa Burkina Faso anayechezea klabu ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Ni miongoni mwa wachezaji waliopendekezwa na kocha Zahera watue Jangwani. Hata hivyo mchezaji huyo anawaniwa na vilabu kadhaa ndani na nje Afrika. Kazi ya ziada itabidi ifanyike kuweza kumpata.

Manji kuongeza nguvu dirisha dogo

Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji ameahidi kuhakikisha wachezaji wote wanaotakiwa na timu hiyo wanasajiliwa wakati wa dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Novemba 15.

Manji aliyeiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya USM Alger mwezi uliopita, ameelezwa kuwa na mkakati kabambe wa kuirejesha Yanga katika anga za Kimataifa.

Kiongozi huyo tayari amerejea Jangwani ingawa kurejea kwake bado hakujawa rasmi kwa kuwa ameomba muda zaidi aweze kuweka mambo yake sawa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’