Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeingia kwenye raundi ya nne leo kwa michezo miwili kupigwa mkoani Shinyanga na jijini Dar es salaam.
Mchezo wa mapema ulikuwa kati ya Mwadui FC dhidi ya Azam uliopigwa dimba la Kambarage mkoani Shinyanga.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 Azam FC ikitangulia kufunga kwa bao la Salum Abubakar kwenye dakika ya 55 huku Mwadui FC ikifanikiwa kusawazisha kwenye dakika ya 71 kupitia kwa Innocent Edwin.
Mchezo uliofuata ilikuwa kati ya African Lyon iliyoikaribisha Coastal Union katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru.
Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Baada ya michezo ya leo, Azam FC imeiondoa Mbao FC kileleni mwa msimamo wa ligi kutokana na wingi wa mabao licha ya timu zote kuwa na alama saba.
Michezo mingine ya mzunguuko wa nne inatarajiwa kupigwa kesho Jumamosi.

Yanga itashuka uwanja wa Taifa keshokutwa Jumapili kuikabili Stand United.

ADVERTISE HERE