Tshishimbi ataibadilisha kabisa Yanga

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
15 Aug 2017
Tshishimbi ataibadilisha kabisa Yanga
Tangu kuondoka kwa Athumani Iddi Chuji na baadae Frank Domayo Yanga haikuweza kupata kiungo mkabaji mwenye uwezo wa kuitendea haki nafasi hiyo.

Wakati huo Chuji akiwa bado 'yuko fiti' alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchezesha timu, alikuwa engine ya Yanga. Pasi zake ndefu ziliwarahisishia kazi mawinga wa Yanga wakati huyo wakiongozwa na Mrisho Ngassa.



Lakini awamu hii Yanga imeleta kiungo ambaye huenda akamaliza kabisa tatizo hilo lililoitesa Yanga kwa miaka kadhaa.

Hapa namzungumzia Papi Kabamba Tshishimbi.

Binafsi nimekuwa nikimfuatilia wakati akiichezea Mbabane Swallows kwenye michuano ya kombe la shirikisho hatua ya makundi ambapo Mbabane ilifanikiwa kutinga.

Tshishimbi ana uwezo mkubwa wa kukaba na kuchezesha timu. Pasi zake nyingi zinafika mahali husika na huyu ni mtaalamu sana wa kupiga pasi ndefu.

Ni mchezaji anayefanya maamuzi kwa haraka, hapendi kukaa na mpira mguuni kwake kwa muda mrefu. Huyu hana muda kabisa na sifa za jukwaani.

Kwa timu yenye washambuliaji wenye kasi kama Yanga ni faida kuwa na mchezaji wa aina yake kwani atawaharakishia kufika langoni.

Aidha kuwasili kwa Tshishimbi kutatoa fursa ya kumuona Thabani Kamusoko akicheza kwenye nafasi yake halisi ya kiungo mchezeshaji.



Naiona 'combination' ya hatari kati ya Tshishimbi, Kamusoko na Raphael Daudi. Uwezo wa hawa jamaa utaimarisha sana kiungo cha Yanga.

Kamusoko na Alpha ni wazuri sana katika kutengeneza nafasi za magoli.



Wakati wao wakitengeneza timu ya kuifunga Yanga (ndio ubingwa wao) Yanga imetengeneza timu ya kutwaa ubingwa wa VPL kwa msimu wa nne mfululizo pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa.

Dhamira hiyo ya Yanga utaiona kwa aina ya usajili wa wachezaji kama Tshishimbi ambaye alikuwa anawaniwa na timu kadhaa Afrika Kusini ikiwemo Orlando Pirates.

Lakini viongozi wa Yanga wamepigania kuhakikisha anatua na kuvaa uzi wa njano na kijani msimu huu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
21h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’