FT : Yanga 4-3 Stand United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Sep 2018
FT : Yanga 4-3 Stand United
Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stand United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa Jumapili jioni uwanja wa Taifa.

Ulikuwa ni mchezo wa aina yake ulioshuhudia idadi kubwa ya mabao saba yakifungwa huku mshambuliaji wa Stand United Alex Kitenge akifunga mabao matatu ikiwa ni 'hat-trik' ya kwanza msimu huu.

Yanga ilianza kuliona lango la Stand United mapema tu kwenye dakika ya pili mfungaji akiwa Mrisho Ngassa 'Uncle' aliyewahi pasi murua ya Ibrahim Ajib.

Kwenye dakika ya 15 Stand United ilisawazisha kupitia kwa Kitenge aliyepiga shuti nje kidogo ya 18 akimshitukiza mlinda lango wa Yanga Klaus Kindoki.



Ajib aliyehusika kwenye mabao yote manne ya Yanga ilifunga bao la pili kwenye dakika ya 31 akipiga shuti kali nje ya 18.

Dakika mbili baadae mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib ulimponyoka mlinda lango wa Stand United kabla ya kumaliziwa kwa kisigino na beki Andrew Vicent na kuiandikia Yanga bao la tatu.

Deus Kaseke akaifungia Yanga bao la nne kwa shuti kali kwenye dakika ya 57 akiwahi mpira uliotengwa kwa kichwa na Ajib.



Kindoki, mlinda lango wa Yanga hakuwa na siku nzuri kwani mpira alioutema kwenye dakika ya 59 ulitua miguuni mwa Kitenge aliyeiandikia timu yake bao la pili.

Kitenge akaifungia Stand United bao la tatu kwenye dakika ya za majeruhi baada ya walinzi wa Yanga na mlinda lango kuzembea kucheza majaro iliyomiminwa kutoka upande wa kulia.

Wakati mchezo huo ukielekea ukingoni Yanga ilipata pigo kwa nahodha wake Kelvin Yondani kuumia na kulazimika kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Ninja.

Licha ya kuibuka na ushindi, ni dhahiri safu ya ulinzi ya Yanga leo haikuwa makini sana kwani iliruhusu kufungwa mabao mepesi.

Mlinda lango Klaus Kindoki alikuwa na 'mchecheto' pengine ni kutokana na kuwa ndio mchezo wake wa kwanza kuanza kuitumikia Yanga kwenye ligi.

Kindoki amekuwa akifanya vizuri kwenye michezo ya kirafiki aliyotumika kabla ya mchezo wa leo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’