Sio jambo la ajabu kwa mchezaji kucheza chini ya kiwango. Hali hii huwa inatokea.
Kwa waliomfuatilia mlinda lango mpya wa Yanga Klaus Kindoki tangu alipotua kuchukua nafasi ya Youthe Rostand watakubaliana nami kuwa ni kipa mzuri sana.
Alionyesha uwezo kwenye michezo ya kirafiki aliyoitumikia Yanga.
Kutofanya vizuri kwenye mchezo mmoja hakumuondolei ubora alionao.
Ni mapema mno kuanza kumlaumu. Mashabiki wakubali kilichotokea ni hali ya mchezo na waendelee kumpa moyo ili asahihishe makosa na aongeze kujiamini.
Tukimtupia lawama tu hatumsaidii yeye na pia hatuisaidii Yanga kwani safari bado ni ndefu. Mbeleni kuna michezo zaidi ya 36, Yanga itawahitaji walinda lango wake wote watatu wawe timamu.
Tujifunze kwa yaliyomkuta Youthe Rostand. Alipotua Yanga mwanzoni mwa msimu alionyesha ubora.
Lakini alipoanza kufanya makosa na mashabiki kuanza kumtupia lawama mfululizo alipoteza kujiamini kabisa.

ADVERTISE HERE