Wachezaji Yanga wapania kushinda kila mchezo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2018
Wachezaji Yanga wapania kushinda kila mchezo
Ushindi wa mabao 4-3 iliyopata Yanga dhidi ya Stand United juzi, umeamsha mzuka wa wachezaji wa mabingwa hao wa kihistoria ambao sasa wamepania kugawa dozi kwa kila anayekuja mbele yao.

Mshambuliaji, Ibrahim Ajibu ambaye juzi alifunga na kuisaidia timu yake kupata ushindi huo, alisema kwa kasi na morali waliyonayo hakuna wa kuwazuia tena.

"Ushindi huu ni muhimu sana kwetu. Kocha anajitahidi kutupa mbinu za kufanya vizuri na tunazifuata," alisema Ajibu.

Aidha, winga wa timu hiyo, Mrisho Ngassa, aliwataka mashabiki kuwaunga mkono kwa sapoti na wao kama wachezaji watapambana uwanjani kupata ushindi.

"Ligi bado mbichi, lakini malengo yetu ni kutwaa ubingwa, wachezaji tutapambana katika kila mchezo kuhakikisha tunafanya vizuri," alisema Ngassa.

Ushindi wa juzi umeifanya Yanga kufikisha pointi sita baada ya kuchezwa michezo miwili mpaka sasa.

Yanga ambayo ipo pointi moja nyuma ya watani zao Simba, lakini ikiwa na mechi moja mkononi, kwa sasa inajiandaa kwa mchezo ujayo wa ligi hiyo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
54m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’