Coastal Union haitasalimika uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2018
Coastal Union haitasalimika uwanja wa Taifa
Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union.

Mchezo huo utapigwa kesho Jumatano saa moja jioni uwanja wa Taifa.

Ukiondoa kipigo cha mabao 8-0 ilichopokea kutoka kwa Yanga mwaka 2015, Coastal Union ni moja ya timu ambazo zimekuwa na kawaida ya kutoa upinzani mkali zinapokutana na Yanga.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika mchezo wa ligi kuu dimba la Mkwakwani, Januari 2016, Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Mabao yaliyofungwa na Miraji Juma na Juma Mahadhi ambaye sasa yuko Yanga.

Baadae mwaka huo mwezi August zikakutana kwenye mchezo wa kombe la FA ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mchezo ukivunjika kwenye dakika ya 105 baada ya mashabiki wa Coastal kuingia uwanjani na kufanya vurugu.

Kwenye mchezo huo Yanga ilisawazisha bao kwatika dakika za majeruhi na kupelekea kuongezwa dakika 30.

Coastal Union iliyorejea ligi kuu msimu uliopita, imeshuka dimbani mara nne, imeshinda mchezo mmoja na kutoka sare michezo mitatu.

Ina alama sita sawa na Yanga lakini ikiwa tayari imecheza michezo minne.

Meneja wa kikosi cha Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema wanatarajia mchezo dhidi ya Coastal Union hapo kesho hautakuwa mwepesi lakini wamejipanga kuibuka na ushindi.

"Coastal Union ni timu nzuri, tunawaheshimu lakini sisi lengo letu ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho ili tufikishe alama tisa," amesema Nadir.

Abdul arejea kikosini

Wakati huo huo nahodha msaidizi wa Yanga Juma Abdul aliyekuwa majeruhi, ameanza mazoezi leo.

Abdul alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Stand United nafasi yake ikichukuliwa na kinda Paul Geofrey.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
25m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
50m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’