Zahera awasimamisha Buswita, Makapu na Haji Mwinyi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2018
Zahera awasimamisha Buswita, Makapu na Haji Mwinyi
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amewasimamisha wachezaji watatu wa klabu hiyo, beki Mwinyi Haji Mngwali na viungo Said Juma Makapu na Pius Buswita kwa utovu wa nidhamu.

Wachezaji hao walimkera kocha Zahera kwa kutozingatia muda juzi, wakati timu inajiandaa kwenda kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United.

Na Zahera ambaye pia kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya DRC akawaondoa kambini na kuwaambia waendelee kutumikia adhabu hadi baada ya mechi ya kesho dhidi ya Coastal Union.

Yanga SC inatarajiwa kuwaalika mabingwa wenzao wa zamani wa Ligi Kuu, Coastal Union katika mchezo uliopangwa kuanza Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa.

Habari njema kuelekea mchezo huo ni kwamba beki Juma Abdul Jaffar Mnyamani aliyekosekana kwenye mechi na Stand United, Yanga ikishinda 4-3 amerejea.

Abdul amefanya mazoezi jana na leo kuelekea mchezo wa kesho unaotarajiwa kuwa mkali kutokana na historia ya kila Yanga inapokutana na Coastal.

Kiungo Juma Mahadhi ndiye pekee hayuko fiti, lakini ameanza mazoezi mepesi ya peke yake.

Kipa Ramadhani Kabwili aliyeondolewa kambini Jumamosi kwa utovu wa nidhamu pia, adhabu yake imeisha na jana na leo amefanya mazoezi.

Kipa Benno Kakolanya aliyekuwa majeruhi amepona na jana na leo amefanya mazoezi pamoja na mlinda mlango, Klaus Kindoki raia wa DRC aliyekuwa langoni juzi, Yanga ikifungwa mabao matatu na Alex Kitenga, japo ilishinda 4-3.

Yanga inahitaji kushinda mechi ya tatu mfululizo nyumbani, baada ya awali kushinda dhidi ya Mtibwa Sugar 2-1 na juzi 4-2 na Stand United.

Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’