Kikosi cha Yanga kiko mafichoni Pemba kujiwinda na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Simba, wiki ijayo August 23.
Yanga imetua Pemba jana Jumatatu siku moja baada ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Kocha wa Yanga George Lwandamina amejinasibu kuwa atatumia kambi hiyo kukiimarisha zaidi kikosi chake na kuhakikisha anarekebisha mapungufu aliyoyaona kwenye michezo ya kirafiki.
Aidha Yanga imeongezewa nguvu baada ya kuwasili kwa kiungo Papi Kabamba Tshishimbi ambaye tayari ametua kisiwani Pemba kuungana na wenzake.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema kikosi hicho kimeanza mazoezi jana jioni kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Simba.
“Tunashukuru Mungu tumewasili salama, na sisi tunaangalia mchezo wetu ujao dhidi ya Simba, kwa hiyo kocha anaendelea na program yake ya mazoezi kujiwinda dhidi ya wapinzani wetu,†alisema.
Wakati Yanga ikijifua Pemba, Simba nayo imetua Unguja kuweka kambi kwa ajili ya mchezo huo pia.

ADVERTISE HERE