Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kiungo Mcongo Papi Tshishimbi amekuwa akifanya kazi kubwa uwanjani inayomfanya achoke sana.
Zahera amesema Tshishimbi anapaswa kutimiza majukumu yake na kupunguza kufanya majukumu ya wengine ili aisaidie timu zaidi.
"Tshishimbi ni mchezaji mzuri lakini anakosa nidhamu ya mchezo. Hatulii sehemu moja. Anakwenda kila mahali hivyo kumfanya achoke sana."
"Anapaswa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati muafaka. Na sio kuwa kila mahali. Pia apunguze mambo ya kupiga chenga. Kazi yake kubwa ni kusambaza mipira, kupora na kutoa pasi kwa wenzie. Ulishawahi kumuona Ng'olo Kante akipiga chenga?," alihoji Zahera.

ADVERTISE HERE