Michezo miwili Ligi Kuu yapigwa leo, Ruvu Shooting yaendelea kupapaswa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Sep 2018
Michezo miwili Ligi Kuu yapigwa leo, Ruvu Shooting yaendelea kupapaswa
Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeendelea leo kwa michezo miwili kupigwa ambapo mkoani Mara Biashara United ilichuana na JKT Tanzania mchezo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Uwanja wa Mabatini kule Ruvu uliwashuhudia wenyeji Ruvu Shooting wakipapaswa na Coastal Union kwa kuchapwa bao 1-0.

Matokeo hayo yanaiacha Ruvu Shooting bila ya ushindi wowote tangu kuanza kwa ligi sasa ikiwa imeingia raundi ya sita.

Kesho Jumapili, Septemba 23 michezo minne inatarajiwa kupigwa kwenye viwanja mbalimbali.

Simba, Mabingwa watetezi ambao wameambulia pointi moja mikoani mpaka sasa watakuwa ugenini mkoani Shinyanga kuikabili Mwadui Fc.

Yanga itakuwa uwanja wa Taifa kuchuana na Singida United kwenye mchezo utakaopigwa saa moja usiku.

Mbeya City itachuana na Kagera Sugar kwenye mchezo mwingine utakaopigwa mapema kwenye dimba la Sokoine huku Alliance ikitarajiwa kuchuana na Azam FC kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’