Licha ya tambo nyingi kutoka kwa msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara anayedai klabu hiyo ndio yenye mashabiki wengi na kufuatiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii, takwimu za mwezi huu zilizotolewa na kampuni ya Results Football zinaonyesha Yanga ndio klabu yenye mashabiki wengi na kufuatiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Yanga iko nafasi ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki huku ikishika nafasi ya 16 barani Afrika ikiwa na jumla ya wafuatiliaji 447,764 kwenye mitandao yake yote ya kijamii.
Inafuatiwa na Gor Mahia iliyo nafasi ya 17 Afrika ikiwa na wafuatiliaji 443,276. Simba iko nafasi ya 19 Afrika ikiwa na wafuatiliaji 392,014

ADVERTISE HERE