FT : Yanga 2-0 Singida United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Sep 2018
FT : Yanga 2-0 Singida United
Mabingwa wa kihistoria Tanzania Bara, Yanga wameendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 baada ya kuilaza Singida United mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa Jumapili usiku uwanja wa Taifa.

Ilikuwa ni siku nzuri kwa Amisi Tambwe aliyerejea rasmi dimbani kukisaka kiatu cha dhahabu msimu huu baada ya kufunga mabao yote mawili ya Yanga.



Tambwe aliifungia Yanga bao la kwanza kwenye dakika ya 29 akimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib.

Hilo lilikuwa bao la tano kutengenezwa na Ajib katika michezo minne aliyocheza akiwa pia amefunga bao moja.

Tambwe huyo huyo akafunga bao la pili kwenye dakika ya 45 kwa shuti la chinichini akimalizia krosi ya Gadiel Michael.




Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa kifua mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili Yanga ilicheza kwa kujihami zaidi huku ikitumia mashambulizi ya kushitukiza.

Tofauti na michezo iliyopita, leo wachezaji wa Yanga walionekana kwenda na kasi ya mchezo katika kipindi cha pili wakijilinda vyema huku wakishambulia kwa kasi kila wanapopata nafasi.

Aidha mlinda lango Beno Kakolanya amedhihirisha kwa nini mashabiki wa Yanga wanataka awe namba moja kwa kuokoa michomo mikali iliyokuwa inaelekezwa langoni kwa Yanga.

Ushindi huo umeiipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 12 kutoka michezo minne.

Yanga pia ina michezo miwili ya kiporo.

Mchezo unaofuta ni Jumapili ijayo, Septemba 30 dhidi ya Simba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’