Kadiri mpambano wa Ngao ya Jamii unavyozidi kukaribia naona upande wa pili wameshaanza kuingia mchecheto.
Hii inatokana na ukweli kwamba wanafahamu ubora wa wYanga pia wameogopa zaidi aina ya ufanyaji kazi wa 'kimyakimya' inayotumiwa na Yanga msimu huu.
Licha ya tambo nyingi, hakuna anayehangaika nao kutoka upande wa Yanga, hiyo pia imewafanya wasielewe wanaandaliwa jambo gani.
Juzi tumemsikia Julio akiwatahadharisha wenzake kuwa wasiichukulie Yanga kiivyo, jana ameibuka nahodha mstaafu wa Simba Jonas Mkude akisema safu ya Ulinzi ya Simba inapaswa ifahamu miongoni wa washambuliaji wa Yanga yupo Ibrahim Ajib.
Mkude amekiri kuwa kukabiliana na Ajib halitakuwa jambo jepesi kwa walinzi wa Simba itabidi wajipange kweli.
Wengine nasikia wameanza kumuhofia Abdallah Shaibu 'Ninja' kuwa huenda akawastaafisha soka washambuliaji wa timu yao ambao wengi ni majeruhi wa kudumu.
Nimemsikia Rage akisema eti watatufunga mabao si chini ya saba! Hiyo ni kauli ya kujipa matumaini tu, anafahamu fika Yanga ya sasa si ya kufungwa saba na Simba.
Kwanza timu yao ina mapungufu makubwa kwenye safu ya ushambuliaji. Wameshindwa kushinda mabao saba walipocheza na kikosi B cha Rayon Sport na wakashindwa pia kufanya hivyo walipocheza na Mtibwa!
Tunawatahadharisha tu, safu ya usashambuliaji ya Yanga ina njaa ya mabao, waangalie tu hizo saba zisije zikawarudia wao.

ADVERTISE HERE