Kiwango kilichoonyesha na kiungo wa Yanga Ibrahim Ajib kwenye michezo minne aliyocheza ya ligi kuu ya Tanzania Bara, kimewatia kiwewe Simba kuelekea mchezo wa kesho.
Ajib 'amezaliwa' upya msimu huu akiwa amehusika kwenye mabao sita kati ya tisa yaliyofungwa na Yanga.
Ndiye kinara wa kutengeneza mabao kwenye ligi kwani katika michezo minne aliyocheza ametengeneza mabao matano na kufunga bao moja.
Kesho anatarajiwa kuingoza Yanga katika mchezo ambao unawakutanisha watani wa jadi utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni kwenye uwanja wa Taifa.
Zahera ampa uhuru
Kutokana na umahiri wake wa kupiga pasi za mwisho kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amempa Ajib uhuru wa kulitawala dimba anavyotaka ili aweze kuinufaisha timu.
Ni dhahiri kutokana na makali aliyoonyesha kwenye michezo iliyopita, Simba itakuja na mkakati wa kumdhibiti lakini haitakuwa rahisi.
Ajib ana kipaji cha hali ya juu na tangu kuwasili kwa Zahera ni kama amejitambua zaidi kwani kocha huyo Mcongomani amemsimamia kikamilifu kuhakikisha anajitambua.
Ajib ana uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi kwa kupiga pasi akiwa katika nafasi yoyote uwanjani. Lakini pia ana umahiri mkubwa katika kutengeneza nafasi za mabao
Kwa sasa 'shughuli' ya Ajib katika kikosi cha Yanga ni kama ile iliyokuwa inafanywa na mkongwe Ronaldinho Gaucho wakati huo akiitumikia FC Barcelona kati ya mwaka 2003 na 2008.

ADVERTISE HERE