Baada ya kukamilisha programu ya mazoezi kwa ajili ya kuwavaa watani zao Simba, wachezaji wa Yanga wamesema kuwa kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kesho na wamewataka mashabiki wao wajitokeze kwa wingi uwanjani.
Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo huo baada ya kumaliza kambi ya siku tano mkoani Morogoro.
Wachezaji hao wamesema wamefanya maandalizi "makubwa" na wapo tayari kwa ajili ya kushuka uwanjani kuchukua pointi tatu muhimu.
Nahodha Kelvin Yondani, amesema kwa sasa kazi waliyobaki nayo ni ya ndani ya uwanja kutokana na kukamilisha maandalizi kama benchi la ufundi lilivyopanga.
Yondani amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi kuwashangalia kwa sababu wamejipanga kuhakikisha wanawapa furaha.
"Tumejiandaa vizuri, mashabiki wetu waje tu uwanjani bila wasiwasi, kocha ametupa mbinu na kazi imebaki kwetu wachezaji," amesema.
Naye winga wa timu hiyo, Mrisho Ngasa, amesema kuwa mchezo huo utakuwa wa ushindani na changamoto mbalimbali lakini hilo hawana hofu ya aina yoyote.
Ngasa ambaye amerejea Yanga akitokea Ndanda FC ya Mtwara amesema anafahamu upinzani uliopo wakati timu hizo zinacheza, lakini mazoezi waliyofanya wakiwa Morogoro yamewasaidia kuwajenga.
Yanga itaumana na Simba huku ikiwa mbele kwa pointi mbili zaidi ya Simba yenye pointi 10 lakini pia kikosi hicho cha Mwinyi Zahera kikicheza mechi moja pungufu.

ADVERTISE HERE