Nyota wa zamani wa Nigeria Emmanuel Amunike anayekionoa kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars amesema amesikia kilio cha Watanzania wanaotaka kuiona timu yao ikifika mbali katika michuano wanayoshiriki na atapambana kwa kutumia nyota wake kufanikisha hilo.
Amunike alisema anajua Watanzania wamekuwa wakiziangalia timu nyingine zikishiriki mashindano mbalimbali, lakini kwa sasa ni muda wa Stars kufanya mambo kama miaka ya nyuma.
βMechi dhidi ya Cape Verde itakuwa sio rahisi kwetu hilo linajulikana, ila nimekuwa nikiongea mara kwa mara na wachezaji tuungane na tujitume kuipigania nchi.
"Hakuna jambo zuri kama kuona nyuso ya furaha usoni kwa mtu wako wa karibu na hilo ndio Watanzania wanakihitaji hivi sasa,β Amunike amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti
Amunike alifunguka zaidi kwa kusema atatumia mbinu tofauti na alizotumia katika mchezo dhidi ya Uganda ili kuhakikisha anapata matokeo dhidi ya Cape Verde.
Cape Verde itacheza na Stars, Oktoba 12 nchini humo kabla ya kurudiana Oktoba 16 wakiwani tiketi ya Fainali ya Afrika (Afcon 2019) zitakazofanyika Cameroon mwakani.
Matokeo ya ushindi au sare kwenye mchezo wa kwanza ugenini yataiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kufuzu kama itashinda michezo yake miwili ya nyumbani.

ADVERTISE HERE