Jana jioni Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Chipukizi ya Pemba na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Bao pekee la Yanga lilifungwa na Ibrahim Ajib. Habari njema zaidi ni kwamba mlinda lango Youthe Rostand alikaa langoni kwenye mchezo huo.
Rostand alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo na sasa baada ya Afya yake kutengemaa upo uhakika kwamba atasimama langoni kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Jumatano ijayo.
Rostand na Kakolanya ndio makipa namba moja wa Yanga huku Ramadhani Kabwili akitarajiwa kutumika kwenye michezo maalumu.
Kakolanya anasumbuliwa na matatizo ya goti na hayuko kwenye kambi huko Pemba.
Kulingana na taarifa iliyotolewa juzi na Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, Geofrey Mwashiuya na Obrey Chirwa nao ni majeruhi hawataweza kuwepo kwenye mchezo dhidi ya Simba.

ADVERTISE HERE