Amunike aahidi Stars 'itapindua meza' uwanja wa Taifa Jumanne

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Oct 2018
Amunike aahidi Stars 'itapindua meza' uwanja wa Taifa Jumanne
Kipigo cha mabao 3-0 ilichopokea Taifa Stars jana kutoka kwa Cape verde kimewakatisha tamaa Watanzania waliokuwa wameanza kujenga imani kwa timu yao baada ya kuonyesha kiwango kizuri michezo iliyopita.

Hata hivyo kocha Mkuu wa timu hiyo Emmanuel Amunike amesema bado wana nafasi ya kukata tiketi ya kufuzu fainali za AFCON 2019 kama watashinda mchezo wa marudiano dhidi ya Cape Verde Jumanne ijayo, Oktoba 16.

Amunike amekiri timu yake haikucheza vizuri jana hasa kwenye kipindi cha kwanza na amesema uzembe uliofanywa na wachezaji wake ulipelekea kufungwa mabao mawili ya haraka haraka kwenye kipindi hicho yaliyowagharimu.

"Tulipoteza mchezo kwenye kipindi cha kwanza. Tuliruhusu mabao mawili mepesi ambayo yametugharimu"

"Kipindi cha pili tulijitahidi. Mchezo huu umekwisha tumepoteza 3-0, lakini tuna mchezo nao nchini Tanzania siku chache zijazo," amesema Amunike.

Amunike amesema watayafanyia kazi mapungu yaliyojitokeza kwenye mchezo huo ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo utakaopigwa dimba la Taifa Jumanne.

Licha ya kufungwa jana, Stars bado ina nafasi ya kufuzu kama itashinda michezo yake miwili ya nyumbani dhidi ya Cape Verde na Uganda.

Cape Verde inaongoza kundi L ikiwa na alama nne sawa na Uganda. Uganda inacheza na Lesotho leo.

Stars ina alama mbili sawa na Lesotho lakini inaburuza mkia baada ya kipigo cha jana.

Timu mbili zitafuzu fainali za michuano ya AFCON mwakani zitakazofanyika mwezi wa sita nchini Cameroon.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’