Uganda yaichapa Lesotho 2-0, Stars hiyooo nafasi ya pili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Oct 2018
Uganda yaichapa Lesotho 2-0, Stars hiyooo nafasi ya pili
Uganda Cranes inahitaji alama moja tu kujihakikishia tiketi ya kufuzu fainali za michuano ya AFCON 2019 baada ya kuilaza Lesotho mabao 2-0.

Mabao ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Faruq Miya yameifanya Uganda ifikishe alama 10 na kuhitaji alama moja tu kimahesabu kutoka michezo miwili ijihakikishie kufuzu.

Aidha matokeo hayo pia yameifanya Stars ichupe hadi nafasi ya pili baada ya kuilaza Cape Verde mabao 2-0 kwenye mchezo wa mapema.

Stars imefikisha alama tano baada ya kushuka dimbani mara nne wakati Cape Verde iko nafasi ya tatu ikiwa na alama nne.

Lesotho inaburuza mkia ikiwa na alama mbili. Imefungwa jumla ya mabao matano na Uganda katika michezo miwili.

Mwezi ujao Stars itasafiri kuivaa Lesotho ugenini wakati Uganda itakuwa nyumbani ikipepetana na Cape Verde.

Kama Stars itashinda mchezo huo na Uganda itaifunga Cape Verde basi timu hizo zitakuwa zimejihakikishia tiketi mapema kabla ya kukutana kwenye mchezo wa mwisho utakaopigwa dimba la Taifa
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’