MO atimiza wiki moja tangu atekwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Oct 2018
MO atimiza wiki moja tangu atekwe
Mfanyabishara Mohammed Dewji ambaye ni CEO wa Makampuni ya MeTL na Muwekezaji wa klabu ya Simba alitekwa Alhamisi iliyopita Hotel ya Coliseum alikokuwa amekwenda Gym kufanya mazoezi.

Leo imetimia wiki moja tangu Bilionea huyo mdogo zaidi Barani Afrika atekwe.

Watanzania kwa pamoja wameendelea kumuombea huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kuchunguza tukio hilo.

Mpaka sasa kulingana na taarifa zilizotolewa na Jeshi la Polisi, watu 27 wamehojiwa huku wengine wakiwa bado wanashikiliwa.

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wanashikiliwa, amewataka Watanzania waendelee kumuombea MO.

"Wiki moja kamili imetimia toka tukio la kutekwa kwa kiongozi wetu MO litokee," Manara ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

"Kwangu mimi binafsi ni tukio baya sana toka nimeanza kazi Simba na Moyo wangu bado umesinyaa

"Tuendelee kumuomba Mola apatikane akiwa Mzima na salama, faraja pekee ninayopata ni kuona Watanzania walio wengi tumeungana kumtakia kheri kiongozi wetu

"Naamini Dua na Sala zetu zitasikika na Insha'Allah kwa jitihada za vyombo vyetu na matakwa yake Mwenyezi,mambo yatakaa sawa"
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’