Yanga yaipania Alliance, yasaka ushindi wa sita

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Oct 2018
Yanga yaipania Alliance, yasaka ushindi wa sita
Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua kwenye uwanja wa chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Alliance.

Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa taifa na unatarajiwa kuanza saa moja kamili usiku.

Tayari wachezaji wa timu hiyo waliokuwa kwenye timu ya Taifa, Kelvin Yondani, Feisal Salum, Gadiel Michael na Beno Kakolanya wamerejea kikosini huku kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera alitarajiwa kutua jana.

Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi itakuwa inasaka ushindi wake wa sita msimu huu na kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo

Katika mchezo huo Yanga itamkosa kiungo wake fundi Feisal Salum 'Fei Toto' anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano huku Andrew Vicent Chikupe naye akitarajiwa kukosekana baada ya kufungiwa michezo mitatu kulingana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni

Tayari Yanga imeweka hadharani viingilio vya mchezo huo ambapo upande wa VIP A ni Tsh 15,000/- VIP B na C Tsh 10,000/- wakati upande wa mzunguuko ni Tsh 5,000/-

Yanga tayari imeshuka dimbani mara sita msimu huu, imeshinda michezo mitano na kutoka sare mchezo mmoja tu.

Imefunga mabao 11 na kuruhusu mabao manne ikiwa na alama 16.

Heritier Makambo, Amissi Tambwe na Ibrahim Ajib ndio vinara wa kupachika mabao kwenye kikosi cha Yanga wakiwa wamefunga mabao mawili kila mmoja.

Ajib ndiye 'engine' ya mabao hayo kwani amehusika kwenye mabao 8 kati ya 11 yaliyofungwa na mabingwa hao wa kihistoria Tanzania
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’