Ajib wapuuze wanaotaka kukuchonganisha na Zahera

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
22 Oct 2018
Ajib wapuuze wanaotaka kukuchonganisha na Zahera
Juzi baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Alliance, Ibrahim Ajib ndiye mchezaji aliyezungumzwa zaidi kutokana na mchango alioutoa kwenye mchezo huo.

Ajib alifunga bao la tatu, lakini pia alitengeneza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Heritier Makambo na Mrisho Ngasa.

Lakini Ajib ndiye mpishi wa mabao ya Yanga kwa asilimia 90. Yanga imefunga mabao 14, amehusika katika mabao 11.

Hata hivyo kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alikuwa na maoni tofauti juu ya mchezaji wake huyo.

Licha ya kumsifia kuwa na kipaji na akili ya soka pengine zaidi ya wachezaji wote wanaoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara, Zahera alimtaka Ajib ajitume zaidi.

Zahera ni kocha aliyekuja na utaratibu tofauti sana. Amekuwa akiwakosoa na kuzungumza mapungufu ya wachezaji wake hadharani

Hata kama timu ikishinda lakini wachezaji wamecheza vibaya yeye hatasifia, atazungumza mapungufu aliyoyaona lengo likiwa ni kuboresha.

Anachokifanya Zahera ni kuwajenga wachezaji wake wasibweteke.

Wakati mwingine sifa zikiwa nyingi sana zinaweza kumfanya mchezaji akajisahau na kujiona amefika.

Ajib ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu, lakini hakosi mapungufu na hayo ndio ambayo Zahera amekuwa akimsaidia kuyaondoa.

Zahera anataka Ajib awe mchezaji 'mkubwa' anae endana na kipaji chake.

Mchezaji ambaye siku za usoni Taifa linaweza kujivunia kama ilivyo kwa akina Samatta, Msuva na wengine wanaosakata kabumbu nje ya nchi.

Mara nyingi Zahera amezungumzia uwezo wa Ajib na amesisitiza kuwa kiungo huyo anatumia sehemu ndogo sana ya kipaji alichonacho.

Kumekuwa na hoja kwa nini AJib hakuitwa timu ya Taifa na kocha Emmanuel Amunike licha ya mafanikio anayoyapata ndani ya Yanga.

Zahera alilizungumzia jambo hilo kitaalamu zaidi na kama Ajib atamsikiliza basi nafasi yake kikosi cha Stars itakuwa inamsubiri.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’