Kikosi cha Yanga kinashuka katika dimba la Taifa keshokutwa Alhamisi kuikabili KMC katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 11.
Yanga itakuwa ugenini kwenye mchezo huo unaotarajiwa kupigwa saa moja usiku.
Kuelekea mtanange huo kocha Mwinyi Zahera amesema hawafikirii kupoteza mchezo wowote wanaocheza katika uwanja wa Taifa.
Katika michezo saba iliyocheza Yanga kwenye dimba hilo, ni Simba pekee iliyofanikiwa kupata sare dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania.
Mtibwa Sugar, Stand United, Coastal Union, Singida United, Mbao Fc na Alliance zote zimechezea vipigo mbele ya Yanga
"Lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika michezo yote tunayocheza hapa Dar es salaam," amesema Zahera
"Matokeo mazuri yatatusaidia kufanya vizuri katika michezo ya mikoani pia kwani morali ya wachezaji itakuwa juu"
Yanga bado ina msururu wa michezo mingi itakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa kutokana na ratiba iliyopangiwa kabla ya kuanza kwenda mikoani.
Kulingana na ratiba, mchezo wa kwanza wa Yanga nje ya Dar utapigwa mkoani Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons Disemba 03, 2018.

ADVERTISE HERE