FT : KMC 0-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Oct 2018
FT : KMC 0-1 Yanga
Yanga imeendeleza wimbi la ushindi kwenye uwanja wa Taifa baada ya leo kuilaza KMC kutoka Manispaa ya Kinondoni kwa bao 1-0.

Mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' kwenye dakika ya 90 uliihakikishia Yanga ushindi muhimu ulioirudisha kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 22.

Fei Toto aliupiga mpira huo kwa ufundi wa hali ya juu ambapo ulienda kujaa pembezoni kabisa upande wa kushoto wa mlinda lango Juma Kaseja.





Ulikuwa ni mchezo uliojaa ushindani kutoka kila upande huku Yanga ikifanya kosakosa za hapa na pale ambapo majaribio kadhaa yaligonga miamba

Wakati mchezo huo ukielekea ukingoni KMC walionekana kuridhika na matokeo ya suluhu ambapo mara kwa mara walifanya jitihada za kupoozesha mashambulizi ya Yanga.



Ushindi huo wa 'usiku' pia umepeleka kilio kwa mashabiki wa Simba ambao tayari walikuwa wameanza kushangilia kwa kudhani mchezo huo ungemalizika kwa matokeo ya sare.

Yanga sasa imeshinda michezo saba kati ya nane iliyocheza kwenye uwanja wa Taifa, ikitoka sare mchezo mmoja tu dhidi ya Simba

Mchezo unaofuata ni dhidi ya Lipuli Fc Oktoba 30 kwenye uwanja wa Taifa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’