Yanga imeanza mazungumzo na beki, Mnyarwanda Abdul Rwatubyaye ikiwa ni harakati zao za kuhakikisha wanaipata saini yake katika dirisha dogo linalofunguliwa mwezi ujao.
Rwatubyaye anaichezea Rayon Sports ya Rwanda aliivutia Yanga wakati timu hizo mbili zilipokutana katika mechi ya hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Beki huyo mrefu mwenye asili ya DR Congo aliwavutia mabosi wa Yanga na haraka mabosi wa kikosi hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hussein Nyika pamoja na aliyekuwa na mjumbe wake, Hamad Islam walinaswa wakifanya maongezi na beki huyo nchini Kigali.
"Yanga ndiyo wameanza mazungumzo rasmi na meneja wangu walinipigia na kutaka mawasiliano naye. Tusubiri kuona kama tutakubaliana na ikiwa hivyo, itabidi pia waongee na Rayon kwa kuwa bado nipo ndani ya mkataba umebaki mwaka mmoja," Rwatubyaye amenukuliwa na Mwanaspoti.
Katika ripoti ya Zahera mbali na kuonyesha anahitaji kiungo na mshambuliaji anahitaji pia beki wa kati.

ADVERTISE HERE