Mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zinazozihusu Azam, Simba na Yanga zilizopangwa kufanyika wiki ya kwanza ya Novemba zimeahirishwa kupisha maandalizi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea mechi dhidi ya Lesotho Novemba 18, mwaka huu kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mechi hizo ni kati ya African Lyon na Yanga iliyopangwa kufanyika Novemba 7, Simba SC na KMC FC na ile ya Azam FC dhidi ya Mbao FC zote Novemba 8, mwaka huu mjini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB), Boniphace Wambura Mgoyo amesema kwamba kutokana na umuhimu wa timu ya taifa, ndio maana wameamua kusogeza mbele michezo hiyo ili kupisha maandalizi hayo.
Amesema kwamba kwa sababu kiu ya kila Mtanzania kwa sasa ni kuona Taifa Stars inakata tiketi ya kucheza AFCON, ndiyo maana Bodi ya Ligi imeamamua kuondoa mechi hizo ili wachezaji waweze kupata muda wa kutosha wa maandalizi katika kambi ya Afrika Kusini.
Lakini pia Wambura amesema kwamba mechi tatu za viporo nazo zimepangiwa tarehe, ambazo ni Novemba 21 Yanga SC na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Simba SC na Lipuli FC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Novemba 22, Azam na Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

ADVERTISE HERE