Zahera amtahadharisha Makambo, benchi linamuita asipobadilika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Oct 2018
Zahera amtahadharisha Makambo, benchi linamuita asipobadilika
Mshambuliaji Heritier Makambo alianza msimu kwa kasi akipachika mabao kwa wastani wa karibu kila mchezo.

Hata hivyo kwa siku za karibuni kasi ya kuzifumania nyavu ya Mcongoman huyo aliyetua Yanga kutoka Fc Lupopo ya DR Congo, imekuwa ndogo

Katika michezo saba aliyoichezea Yanga kwenye ligi, Makambo amefunga mabao matatu sawa na kiungo Ibrahim Ajib.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemtaka mshambuliaji huyo aongeze juhudi na kuhakikisha anazitumia ipasavyo nafasi anazopata kabla benchi halijamuita.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi baada ya mchezo dhidi ya KMC, Zahera aliyekuja na utaratibu wa kuwakosoa wachezaji wake hadharani, alisema hakufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji huyo.

Zahera alisema amemtahadharisha mshambuliaji huyo na kumtaka abadilike. Na kama hatabadilika hatamtumia katika michezo ijayo.

"Nimemwambia abadilike, aache mambo yake ya hovyo. Afanya mazoezi vizuri ale vizuri na alale vizuri. Akiendelea kucheza vibaya hatapata nafasi kwenye timu yangu," alisema

Yanga itashuka tena dimbani Jumanne ijayo kuikabili Lipuli Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 12.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’