Afisa Habari wa klabu ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amethibitisha kuwa aliyekuwa Kiungo wa timu hiyo Mohammed Issa 'Banka' alimaliza mkataba wake wa kuitumikia Mtibwa Sugar.
Kifaru amesema Mtibwa Sugar ilikuwa na mpango wa kumuongezea mkataba mwingine kwa manufaa ya baadae ya klabu hiyo lakini hawakufikia muafaka kutokana na mchezaji mwenyewe kuonesha nia ya kuondoka klabuni hapo.
Kifaru amesema hayo baada ya shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF kudai kuwa wanamtambua Mo Banka kama ni mchezaji Mtibwa Sugar wakati wakitangaza kuwa mchezaji huyo amefungiwa miezi 14 kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya Bangi.
Katika hatua nyingine Afisa Habari wa Yanga Sc Dismas Ten amesema walimsajili Mo Banka kwa kufuata taratibu zote za usajili na jina lake lilikubaliwa kwenye system ya usajili ya TFF lakini hawakufanikiwa kupata leseni ya mchezaji huyo kutokana na sakata la kufungiwa kwake.
Ten amesema wanasubiri barua rasmi kutoka kwa TFF baada ya kufungiwa kwa Mo Banka kabla ya kutoa taarifa rasmi ya klabu.

ADVERTISE HERE