Taarifa ya TFF kuhusu agizo la uchaguzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Nov 2018
Taarifa ya TFF kuhusu agizo la uchaguzi Yanga
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Jumapili Novemba 4, 2018 kujadili kuhusu uchaguzi wa Young Africans.

Kamati inaiagiza Klabu ya Young Africans kufanya Uchaguzi wake Januari 13,2019 ikiwa ni siku 60 kwa mujibu wa kanuni ya Uchaguzi.

Nafasi watakazotakiwa kuzijaza ni nafasi ya Mwenyekiti ,nafasi ya Makamu Mwenyekiti aliyepoteza sifa katika nafasi hiyo na nafasi 4 za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao walijiuzulu.

Kwa mujibu wa kalenda ya Uchaguzi Novemba 5-7,2018 kutangaza mchakato wa Uchaguzi wa Young Africans na kubandika kwenye Mbao za matangazo,zoezi ambalo litafanywa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Novemba 8- 13,2018 kuchukua na kurudisha fomu za kuomba uongozi,fomu ambazo zitatolewa Makao Makuu ya Klabu ya Young Africans na fomu nyingine zitapelekwa Makao Makuu ya TFF Karume,Ilala kwa wengine kuchun kulia hapo.

Novemba 21-22,2018 itakuwa kipindi cha kuweka pingamizi kwa Wagombea

Novemba 24-27,2018 itakuwa kipindi cha kupitia mapingamizi na kufanya usahili wa Wagombea,zoezi ambalo litafanywa na Kamati ya Uchaguzi.

Novemba 28-30,2018 kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usahili.

Orodha ya mwisho ya Wagombea itachapishwa,kutangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo Januari 3-5,2019.

Kipindi cha Kampeni kwa Wagombea kitakuwa kuanzia Januari 6-11,2019.

Katakana na mapungufu ya kamati ya utendaji na mapungufu ya kamati ya uchaguzi ya Young Africans , na kwa kuzingatia maelekezo ya Baraza la Michezo la Taifa , uchaguzi huu utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kushirikiana na Uongozi wa Young Africans,Zoezi hili utekelezaji wake ni mara moja.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’