Wazambia wamtaka Zahera, mwenyewe asema haondoki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Nov 2018
Wazambia wamtaka Zahera, mwenyewe asema haondoki Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amethibitisha kutia nanga ndani ya kikosi hicho kwa kauli yake kwamba hata angepewa dola 40,000 hawezi kuondoka.

Hayo ameyasema siku chache baada ya uongozi wa Yanga kuthibitisha kupokea simu kutoka moja ya timu ya Ligi Kuu Zambia wakiomba mazungumzo kuhusu kuwauzia kocha huyo ambaye ana mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Zahera ambaye tayari ametimka nchini na kwenda kujiunga na timu ya Taifa ya Congo akiwa kama Kocha Msaidizi alisema hawezi kuiacha Yanga hata ikiwa katika hari mbaya vipi, kwani yeye haamini kama maisha ni pesa pekee bila utu.

β€œMimi kama mwalimu nimekuwa nikiwasisitiza wachezaji wangu kila siku kuhakikisha wanavumilia hali wanayokumbana nayo sasa katika klabu yao, nawaambia wapambane kuibeba timu naanzia wapi kuwaakimbia naondoka kisa maslahi,”

β€œNi kweli nimeambiwa na uongozi kuwa kuna timu kutoka Zambia, mimi sijajua ni timu gani wamewapigia simu kuwaomba niende kuifundisha timu yao kiukweli sipo tayari kuwaacha wachezaji wangu na kuiacha Yanga, nitaondoka nikifukuzwa au Yanga ikifa,” alisema.

Zahera aliongeza kuwa ameikuta timu hiyo ikiwa vibaya kiuchumi na aliweza kukubaliana na hali hiyo kwa kuingia mkataba wa miaka miwili, hivyo hawezi kuikimbia kwa sababu hata akitoka Yanga na kwenda Zambia huenda akakutana na changamoto kama hiyo.

β€œHao viongozi kutoka Zambia wanaweza wakanitafuta sasa wakiwa na uwezo mzuri wa fedha na baadaye wakakosa hiyo fedha nitakimbilia wapi tena, nitaendelea kubaki Yanga kwa hali yoyote sina tabia ya kuangalia maslahi zaidi huwa na utu ni muhimu kwangu,” alisema.

Zahera alijiunga Yanga akiziba nafasi ya aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, George Lwandamina ambaye aliikimbia klabu hiyo kutokana na ukata uliowakumba na kuamua kurudi katika timu yake ya zamani ya Zesco ambayo ndio anaitumikia hadi hivi sasa
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’