Uongozi wa Azam Fc umemalizana na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Obrey Chirwa aliyerejea Tanzania baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nogoom El Mostakbal FC inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri.
Chirwa amekamilisha usajili wake na klabu ya Azam Fc kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
Anasubiri kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili wiki ijayo aweze kusajiliwa rasmi na kuanza kuitumikia timu hiyo inayonolewa na Hans van Pluijm kocha aliyewahi kuinoa Yanga kwa mafanikio makubwa.

Yanga ilikuwa na nafasi ya kumsajili tena mshambuliaji huyo. Hata hivyo kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera alimkataa akieleza kutofurahishwa na mwenendo wake wa utovu wa nidhamu.

ADVERTISE HERE