Mlinda lango wa Yanga Beno Kakolanya alipata majeraha jana katika mazoezi ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' yanayoendelea nchini Afrika Kusini.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, Kakolanya aligongana na mshambuliaji wa Azam Fc Yahya Zayd na wote wawili kuumia.
Msemaji wa TFF Cliford Ndimbo amesema wachezaji hao wanaweza kurejea mazoezini kesho asubuhi.
Wakati huo huo Ndimbo amesema wachezaji wa Stars wanaosakata kabumbu nje ya nchi wanatarajiwa kuanza kuwasili kambini nchini Afrika Kusini keshokutwa Jumapili
Stars imeendelea kujifua huko Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 dhidi ya Lesotho utakaopigwa Novemba 18 huko Maseru, Lesotho.

ADVERTISE HERE