Pamoja na kuthibitisha kuwa Yusuff Manji ni Mwenyekiti halali wa Yanga baada ya yeye mwenyewe kuandika barua ya kuridhia kurudi, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Kapteni George Mkuchika ameitaka Kamati ya Utendaji ya Yanga kukutana na TFF ili kupata mwafaka wa hatma ya uchaguzi nafasi ya Mwenyekiti.
Katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Januari 13 2019, nafasi ya Mwenyekiti ni miongoni mwa nafasi zilizotangazwa kujazwa.
Nyingine ni Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
Kapteni Mkuchika amesema Baraza la Wadhamini linakubaliana na uchaguzi huo kufanyika lakini limeiagiza Kamati ya Utendaji kukutana na TFF ili kuthibitisha kurejea kwa Manji kupitia ushahidi wa barua yake aliyoandika.

ADVERTISE HERE