Shirikisho la soka nchini (TFF) limesema Jeshi la Polisi limewahakikishia kuwa usalama utakuwa wa kutosha kwenye dimba la Taifa katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas alisema takribani Askari 300 watakuwepo kwenye dimba la Taifa kulinda Amani.
Lucas alisema miongoni mwa Askari hao watakuwepo wenye mbwa, farasi na wale wa kawaida.
Mchezo wa Ngao ya jamii unatarajiwa kupigwa Jumatano, August 23 kwenye dimba la Taifa kuanzia saa 11 jioni ukihusisha timu kongwe na zenye mashabiki wengi zaidi nchini Tanzania.
Yanga ikiwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa misimu mitatu mfululizo itaumana na Simba, mabingwa wa kombe la FA (ASFC).

ADVERTISE HERE