Yanga iongeze mshambuliaji sawa, lakini Tambwe asikatwe

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
15 Nov 2018
Yanga iongeze mshambuliaji sawa, lakini Tambwe asikatwe
Dirisha la usajili limefunguliwa rasmi leo Alhamisi Novemba 15 na linatarajiwa kufungwa baada ya mwezi mmoja.

Wakati huu mabosi wa Kamati ya Usajili ya Yanga wako 'busy' kukamilisha usajili wa wachezaji waliopendekezwa na kocha Mkuu Mwinyi Zahera.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amethibitisha kuwa yuko 'kazini' kukamilisha usajili wa wachezaji hao akianza na wale wanaocheza ndani.

Miongoni mwa nafasi ambazo zilipendekezwa na Zahera ni pamoja na kuongeza mshambuliaji mwingine atakayesaidiana na Mcongomani Heritier Makambo

Hata hivyo kumekuwa na taarifa kwamba Yanga huenda ikaachana na mshambuliaji wake, kinara wa mabao katika kipindi cha misimu mitano iliyopita, Amissi Tambwe.

Tangu apate majeraha ya goti mwishoni mwa msimu wa 2016/17 Tambwe amekuwa na wakati mgumu kurejesha makali yake.

Msimu uliopita alionekana dimbani mara chache sana, kutokana na majeraha hayo ambayo ilimlazimu afanye kazi ya ziada ili aweze kupona.

Kuna wakati Tambwe alifanyiwa maombi maalum ili aweze kupona.

Kwa sasa Tambwe amepona kabisa majeraha hayo na msimu huu ameweza kucheza karibu michezo yote ingawa mingi amekuwa akiingia kwenye kipindi cha pili.

Yanga itafanya makosa makubwa sana kama itamuacha Tambwe ambaye Oktoba 24 alitimiza miaka 30.

Wakati kocha Zahera akimuamini zaidi Makambo, lakini mshambuliaji huyo amekuwa akikosa nafasi nyingi za wazi.

Alichoongeza Makambo kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga ni uwezo wake wa kumiliki mpira na usumbufu wake kwa mabeki.

Lakini ukizungumzia 'shabaha' ya kuzifumania nyavu, hakuna ubishi Tambwe ni zaidi yake.

Kama Zahera angeamua kuwatumia wote wawili katika michezo mingi pengine Yanga ingefunga mabao mengi zaidi kuliko sasa.

Anachohitaji Tambwe baada ya kukaa nje kwa mda mrefu ni mazoezi ya kumsaidi aweze kuwa 'fit' na naamini kocha Zahera na benchi lake la ufundi wanaweza kumsaidia

Hali kama hiyo ilimkumba Mzimbabwe Thabani Kamusoko ambaye kiwango chake kimeanza kurejea taratibu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’