Baada ya kukamilisha usajili wa Donald Ngoma na Obrey Chirwa, Azam Fc inadaiwa kuwa mbioni kumsajili kiungo wa Simba Haruna Niyonzima.
Inadaiwa Niyonzima aliye kwenye mgogoro na uongozi wa Simba kuhusiana na masuala ya mikataba, anataka kuvunja mkataba wake na huenda akaelekea Azam Fc baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa timu hiyo.
Kama usajili wake utafanikiwa mchezaji huyo atakuwa wa tatu kutua Azam fc kuungana na kocha Hans van Pluijm.
Tangu atue Azam Fc akitokea Singida United, Pluim amesajili wachezaji wengi aliofanya nao kazi katika vilabu tofauti.
Singida United aliondoka na Mudathir Yahya, Tafadzwa Kutinyu na Dani Lyanga kwenda Azam Fc.
Wakati alipoondoka Yanga kwenda Singida United aliondoka na Deus Kaseke na Ali Mustafa 'Barthez'.
Pia kocha huyo raia wa Uholanzi alimteua Juma Mwambusi aliyefanya nae kazi Yanga kuwa kocha wake msaidizi.
Tayari amewasajili Ngoma na Chirwa na sasa anakaribia kumnyakua Niyonzima wachezaji wote akiwa amefanya nao kazi Yanga.

ADVERTISE HERE