Winga Emmanuel Martin huenda akaondoka Yanga kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo baada ya Tanzania Prisons kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.
Tangu atue kocha Mwinyi Zahera, Martin amekuwa na nafasi finyu ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza akishindwa hata kuwa miongoni mwa wachezaji wa akiba kwenye michezo yote 10 ya ligi ambayo Yanga imeshacheza mpaka sasa.
Klabu ya Prisons inataka kumsajili mchezaji huyo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake ambacho kimekuwa na mwendo wa kusuasua msimu huu.
Uwezekano wa Martin kuondoka Yanga ni mkubwa kwani mwenyewe amesisitiza anahitaji kupata nafasi zaidi ya kucheza ili kulinda kiwango chake.
Mkataba wake na klabu ya Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu.

ADVERTISE HERE