Yanga kuifuata Mwadui Fc Jumanne ijayo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Nov 2018
Yanga kuifuata Mwadui Fc Jumanne ijayo
Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wiki ijayo kwa michezo ya viporo ambapo mabingwa wa kihistoria Yanga, Novemba 22 watakuwa mkoani Shinyanga kuikabili Mwadui Fc.

Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam siku ya Jumanne Novemba 20 kwa usafiri wa Ndege.

Uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa Afisa habari wake Dismas Ten, umesema maandalizi ya safari hiyo yamekamilika.

kabla ya kwenda Shinyanga, Yanga itaelekea mkoani Lindi ambapo Jumapili ijayo itachuana na Namungo Fc kwenye mchezo wa kirafiki.

"Kama ambavyo unafahamu, Jumapili timu yetu itakuwa Lindi kwenye uwanja wa Majaliwa, kucheza mchezo wa kirafiki na Namungo Fc, baada ya mchezo huo tunatarajia kikosi kitarejea Dar siku ya Jumatatu asubuhi na Jumanne alfajiri itasafiri kwenda Shinyanga, kwa ajili ya mchezo wa ligi siku ya Alhamisi," amesema Ten

"Mwadui ni timu nzuri wamekuwa wakipata matokeo wanapocheza nyumbani, tunafamu hilo ndiyo sababu tumefanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kupima uwezo wetu, imani ya kila mmoja klabuni kwentu ni kuwa tunakwenda kupambana ili tupate matokeo mazuri."

Ten amesema kocha Mwinyi Zahera atauwahi mchezo huo dhidi ya Mwadui Fc kwani anatarajiwa kuwasili siku ya Jumatatu

"Mwalimu alikuwa Congo DRC kwenye majukumu ya timu ya taifa, atarejea nchini Jumatatu jioni kwa ajili ya safari, hakuna shaka yoyote juu yake kwa wote tunafahamu juu ya majukumu aliyonayo kwenye taifa lake lakini pia umuhimu mkubwa alionao na anaoutoa kwa timu yetu."

Wakati huo huo kiungo Juma Mahadhi ameanza mazoezi mepesi baada ya kukosekana dimbani tangu mwezi wa nane.

Mahadhi aliyekuwa nje kwa miezi mitatu, ameanza mazoezi mepesi kabla ya kurejea rasmi dimbani
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’