Ekerege afunguka, Yanga bila Manji haitavuka salama kipindi hiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2018
Ekerege afunguka, Yanga bila Manji haitavuka salama kipindi hiki
Meneja wa zamani na mwanachama wa Yanga, Robert Ekerege ameibuka na kuwaambia Wanayanga kwamba hakuna namna nyingine ya kumaliza matatizo ya kifedha ndani ya klabu yao zaidi ya uwepo wa Yusuf Manji kwasasa.

Yanga ipo kwenye mchakato wa uchaguzi ingawa bado kuna mvutano kati ya klabu hiyo na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ambao sasa ndiyo wanaendesha mchakato huo kwa maagizo ya serikali kwamba wasimamie kwa vile Kamati ya Utendaji ya Yanga haijatimia kwani wajumbe wengi walijiuzulu.

Yanga wanamuhitaji Manji ambaye mwaka jana aliandika barua ya kujiuzulu ambapo wanachama waligoma na kwamba wanamtambua kama Mwenyekiti wao na awali TFF ilibariki maamuzi hao ya wanachama wa Yanga ingawa sasa hawatambui na kuwataka nafasi yake ijazwe kupitia uchaguzi huo.

Ekerege aliliambia gazeti la Mwanaspoti kuwa wanachama na wadau wengi hawafahamu undani wa tatizo la Yanga kwani hivi sasa hakuna mtu ambaye anaweza kuingia Yanga na kulipa madeni yote hasa ya wachezaji wao.

Kwani waliowengi uwezo wao ni wa kawaida na hawapo tayari kujitolea.

"Manji hana nia ya kukaa Yanga milele, jambo pekee ambalo wanapaswa kulifahamu ni kwamba uwepo wa Manji utaisaidia klabu kuvuka kwenye kipindi hiki kigumu ikiwemo kutusaidia kusajili wachezaji wa maana vinginevyo hizi propaganda zikiendelea itakula kwetu, dirisha la usaliji litafungwa tutabaki hivi hivi.

"Manji amekubali kurejea Yanga na sio kwamba anahitaji kiivyo kukaa Yanga na uhitaji wake ni tofauti na Yanga inavyomuhitaji Manji na hiyo yote ni kwavile amekuwa na msaada mkubwa ndani ya Yanga.

"Wamruhusu Manji afanye kazi yake kwa miaka miwili ijayo wakati tunajipanga, muda ukifika wa kufanya uchaguzi tutafanya kwani akiwa anaendelea na madaraka yake tutakuwa tunaendelea na mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji maana hiyo ndiyo njia pekee ya kujikwamua, hata yeye ndiyo malengo yake," alisema Ekerege.

Uchaguzi wa Yanga unatarajia kufanyika Januari 13 mwakani huku wagombea zaidi ya 22 wakijitokeza kuchukuwa fomu nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’