Pluijm aitabiria ushindi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
23 Aug 2017
Pluijm aitabiria ushindi Yanga
Kocha wa Singida United Hans van der Pluijm, ameitabiria ushindi klabu ya Yanga wakati kesho itakaposhuka dimbani kupambana na mahasimu wao Simba kwenye pambano la Ngao ya Jamii.

Katika mahojiano na mtandao wa GOAL Pluijma ameeleza sababu ya kuipa Yanga nafasi ni kutokana na ukali wa safu yao ya ushambuliaji pamoja kiungo chao kuimarika kuliko ilivyokuwa wakati wanaanza maandalizi ya msimu huu.

“Mchezo utakuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa lakini nawapa nafasi Yanga, kwa sababu ni timu ambayo ina safu kali ya ushambuliaji na wana watu wazuri kwenye eneo la kiungo ambao wanauwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wao,”amesema Pluijm

Kocha huyo amesema kitakacho waua Simba ni staili yao ya uchezaji ya kupiga pasi nyingi wakiwa kwenye eneo la ulinzi kitu ambacho kinaweza kuwaponza kwani washambuliaji wa Yanga niwepesi na wanaweza kuzitumia vizuri nafasi wanazozipata.

Amesema kitu kingine kibaya kwa Simba ni ubutu wa safu yao ya ushambuliaji ambayo licha ya kutengeneza nafasi nyingi lakini imekuwa ikifunga mabao machache.

“Tusubiri kuona lakini Simba wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na matatizo mengi kuliko Yanga, na mbaya zaidi wanajidanganya, kuwa wanatimu nzuri zaidi ya Yanga lakini ukweli watauona kesho,”amesema Pluijm.

Pluijm amewahi kuwa kocha wa Yanga kwa vipindi viwili tofauti na ndiye aliyetengeneza kikosi cha Yanga ambacho kimerithiwa na kocha George Lwandamina msimu uliopita.

Lwandamina amefanya marekebisho madogo kwenye kikosi hicho alichoachiwa na Pluijm ambapo msimu huu amesajili wachezaji tisa.

Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki na Singida United na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →