African Lyon imeongeza idadi ya timu zinazowania baadhi ya wachezaji wa Yanga baada ya kuitaka huduma ya kiraka Pato Ngonyani kwa mkopo
African Lyon ilijaribu kumsajili Pato tangu wakati wa usajili wa dirisha kubwa uliofungwa Julai 26 lakini ikashindwa kufikia makubaliano na uongozi wa Yanga
Pato ameshindwa kuingia kwenye kikosi cha Mcongomani Mwinyi Zahera hivyo huenda akaruhusiwa kujiunga na timu hiyo kama makubaliano yatafikiwa.
Wakati Pato akitakiwa na African Lyon, Prisons imetaka kumsajili Emmanuel Martin ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu.
Polisi Tanzania nayo inawanyemelea Yusufu Mhilu na Yohana Mkomola kwa mkopo.
Hata hivyo hatma ya wachezaji hao iko mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera ambaye ndiye atakayetoa mapendekezo juu ya mustakabali wao.
Bado uongozi wa Yanga haujaweka wazi wachezaji ambao imewasajili mpaka sasa ingawa inafahamika iko kwenye michakato ya kukamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji hao.
Miongoni mwao ni mshambuliaji kutoka Uganda Nelson Senkatuka ambaye imeelezwa atakuja nchini wiki hii kumalizana na uongozi wa timu hiyo.

ADVERTISE HERE